Waliomsimamisha masomo Abdul Nondo kuburuzwa mahakamani

Image result for abdul nondo1650x450-mega-promotions_3

Taasisi ya watetezi wa haki za binadamu Tanzania, THRDC imeuomba uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) kumrudisha mara moja masomoni Mwanafunzi wa chuo hicho ambaye pia ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini (TSNP) kwani kupata elimu ni haki yake ya msingi.

Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa amesema kuwa wataandika barua ya kuuomba uongozi wa UDSM kufuta adhabu waliyompa Abdul Nondo ya kusimamishwa masomo kwa hadi kesi yake itakapomalizika na endapo watashindwa kufanya hivyo basi, THRDC watachukua hatua za kuufikisha uongozi huo mahakamani kudai haki zaidi.

Juzi Machi 26, 2018 Uongozi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), ulitoa taarifa ya kumsimamisha masomo, Abdul Nondo hadi kesi mbili zinazomkabili mkoani Iringa za kutoa taarifa za uongo mtandaoni na kudanganya kutekwa zitakapomalizika.

BARIKIWA NA WIMBO WA HANCE PETER SAA IKIFIKA

Leave a comment