AFYA: FAHAMU DAWA MBADALA 10 ZINAZOTIBU MAUMIVU YA KICHWA

 

Je unasumbuliwa na maumivu ya kichwa kila mara? Inakupelekea kichwa kuuma na kujisikia kuchoka sana? Na je unahitaji kujua namna unavyoweza kuondoa maumivu haya haraka kadri inavyowezekana?

Kama jibu lako ni ndiyo basi endelea kusoma makala hii hadi mwisho ambapo naenda kukuonyesha dawa za asili 10 unazoweza kuzitumia kujitibu na maumivu yako ya kichwa bure tu hulipi hata 100.

Utakumbuka kama wiki 1 hivi iliyopita nilikuletea somo juu ya dawa za asili zinazotibu kipanda uso.

Katika makala hii nimekukusanyia pamoja na maelezo yake dawa mbadala 10 unazoweza kutumia nyumbani kujitibu na maumivu ya kichwa.

Kumbuka maumivu yakizidi muone daktari kwa uchunguzi zaidi.

Dawa mbadala 10 zinazotibu maumivu ya kichwa

1. Juisi ya mnanaa (Mint Juice)

dawa nyingine ya asili ya kutibu maumivu ya kichwa ni juisi ya mnanaa kwakuwa mnanaa una vitu viwili vinavyosadikiwa ndiyo vinahusika na kutoa maumivu ya kichwa vijulikanavyo kama ‘menthol’ na ‘menthone’.

Namna ya kutumia sasa hii dawa:

Mahitaji:

* Mkono mmoja wa majani freshi ya mnanaa

Namna ya kuandaa:

* Kwanza twanga kwenye kinu hayo majani mpaka yalainike.
* Kisha pakaa haya majani sehemu ya mbele ya kichwa chako na uache hapo kwa dakika 20 hivi.

Fanya zoezi hili mara 1 au 2 kwa siku.

Unaweza pia kutumia mvuke uliotokana na chai ya majani ya mnanaa ukijifukiza sehemu ya mbele ya kichwa chako ili kupata nafuu ya haraka.

2. Tangawizi

Tangawizi inajulikana kama dawa nzuri kwa kutibu maumivu ya kichwa. Inachofanya tangawizi ni kupunguza maambukizi kwenye mishipa yako ya damu.

Kuna namna mbili unaweza kutumia tangawizi kutibu maumivu ya kichwa.

Moja ni kutengeneza juisi ya tangawizi, kipande kidogo tu cha tangawizi tumia maji na blenda tengeneza juisi yake upate kikombe kimoja na uchuje kisha ongeza vijiko vikubwa viwili vya maji maji ya limau na asali kidogo kupata radha na unywe kutwa mara 1 kwa siku kadhaa mpaka maumivu yameisha.

Namna ya pili ni kutengeneza chai ya tangawizi ukitumia tangawizi, maji na asali kama ndiyo sukari yako.

Kunywa chai hii kikombe kimoja kutwa mara 1 au 2 kwa siku kadhaa.

Unaweza pia kutafuna kipande kidogo cha tangawizi kupunguza maumivu hayo.

Tangawizi isitumike kwa wingi kwa mtu anayetafuta ujauzito au mwenye mimba changa.

3. Kipande cha barafu

Barafu ni aina nyingine ya dawa ya asili isiyo na gharama ya kutibu maumivu ya kichwa. Kipande cha barafu kinasaidia kupunguza muwako au joto vitu ambavyo ni moja ya vitu vinavyoweza kusababisha maumivu ya kichwa.

Barafu pia ni nzuri kurekebisha hali ya maumivu.

Unaweza kutumia kipande cha barafu kuondoa maumivu ya kichwa kwa namna hizi mbili zifuatazo:

* Kwanza weka kipande cha barafu katika kitambaa kisafi na uweke nyuma ya shingo yako kwa dakika kadhaa. Hii njia itakuondolea maumivu haraka sana.

* Namna nyingine ni kuweka kitambaa safi ndani ya maji ya baridi sana kama barafu kisha funika sehemu ya mbele ya kichwa chako na kitambaa hiki kwa dakika 5. Unaweza kufanya zoezi hili mara kadhaa kwa siku mpaka maumivu yamepotea.

4. Mrehani

Unaamini kuwa mrehani (basili) unaweza kukusaidia kuondoa maumivu yako ya kichwa kwa haraka? Hii ni kwa sababu sifa ya kutuliza maumivu (analgesic properties) ipatikanayo kwenye mrehani inaweza kusaidia kutuliza kichwa chako.

Kutibu maumivu ya kichwa kwa kutumia mrehani tumia njia zifuatazo:

* Tengeneza chai ukitumia majani freshi ya mrehani.

* Chemsha maji kikombe kimoja (robo lita) kisha ipua na tumbukiza majani matatu mpaka manne ya mrehani na uache kwa dakika kadhaa.

* Ongeza asali kidogo kupata radha kisha kunywa chai hiyo ili kuondoa maumivu ya kichwa.

Unaweza pia kuchemsha hayo maji sambamba na majani ya mrehani ndani yake kama unavyofanya kupika chai nyingine ya kawaida.

• Au unaweza pia kutafuna tu majani kadhaa ya mrehani moja kwa moja mabichi hivyo hivyo mara kadhaa kwa siku. Unaweza pia ukipata mafuta ya mrehani ukapakaa kwenye paji la uso mara kadhaa kwa siku ili kuondoa maumivu haya ya kichwa.

Uchaguzi ni wako.

Hizo zote hapo juu ni dawa za asili za kuondoa maumivu ya kichwa ambazo unapaswa kuzijaribu.

Endelea kusoma makala hii kwa dawa nyingine zaidi.

5. Karafuu

Kwa vile karafuu ina sifa ya kukufanya mtulivu na kukuondolea maumivu mbalimbali basi ninaiandika hapa kama dawa ya asili unayoweza kuitumia kuondoa maumivu yako ya kichwa ambayo unatakiwa uijaribu pia.

Hivyo unaweza kutumia karafuu kuondoa maumivu yako ya kichwa.

Tumia kwa namna zifuatazo:

* Kwanza chukua karafuu kadhaa na uzitwange kidogo ila zisiwe unga, kisha zifunge kwenye tishu. Muda wowote kichwa kikiuma sogeza karibu na pua yako na unusenuse mara kadhaa mpaka maumivu yametulia.

* Namna nyingine ni kuchukua mafuta ya karafuu na ufanye masaji ya kichwa ukitumia mafuta haya.

* Unaweza pia kuchanganya matone mawili ya mafuta ya karafuu, kijiko kidogo kimoja cha chai cha chumvi na vijiko vidogo viwili vya mafuta ya nazi. Tumia mchanganyiko huu kufanya masaji ya kichwa na ya paji la uso kuondoa maumivu ya kichwa.

Tumia njia hizo ukitumia karafuu kutibu maumivu yako ya kichwa.

6. Siki ya tufaa

Tunda lenyewe na hata siki yake vinaweza kutumika kutuliza maumivu ya kichwa sababu ya uwezo wake wa kuweka sawa usawa wa tindikali na alkalini kwenye mwili wako.

Siki ya tufaa (Apple cider vinegar) inatumika na watu wengi duniani kama dawa ya asili kutibu maumivu ya kichwa.

Kama unasumbuliwa na kuumwa kichwa mara kwa mara unaweza kula tunda hili sambamba na chumvi kidogo kisha unywe maji ili kutuliza maumivu hayo.

Vile vile unaweza kuongeza kijiko kidogo kimoja cha siki ya tufaa ndani ya maji kikombe kimoja na unywe kutwa mara 2 kwa siku kadhaa kutibu maumivu yako ya kichwa.

7. Limau

Pamoja na dawa nyingine nilizokupa hapo juu sijataka kusahau kukueleza kuhusu limau inavyoweza kukuondolea maumivu ya kichwa kirahisi zaidi sababu limau inayo sifa ya kukufanya mpole na mtulivu kwa asili kabisa bila madhara yoyote kama vile ungetumia dawa za kizungu.

Limau linasemwa huondoa mfadhaiko wa akili (stresss) na kukuacha mpole na mkimya. Limau linaondoa asidi iliyozidi mwilini pia lina vitamini C ya kutosha.

Namna rahisi ni kukamua maji maji ya limau 1 au nusu yake kisha changanya na maji ya uvuguvugu kikombe kimoja na unywe yote kutwa mara 1 au 2 kwa siku kadhaa.

8. Mdalasini

Unafikiri mdalasini ni dawa nyingine nzuri kwa kutibu maumivu ya kichwa? Kama ndiyo basi upo sahihi.

Mdalasini hutumika kutibu maumivu ya kichwa hasa yale yaliyotokana na hewa ya baridi sana.

Namna ya kutumia; chukua mdalasini ya unga kijiko kikubwa kimoja, ongeza maji kidogo kupata uji mzito (paste) kisha pakaa uji huu kwenye paji la uso na uache hapo kwa dakika 30 hivi kisha jisafishe na maji ya uvuguvugu.

Fanya hivi mara 2 kwa siku kwa siku kadhaa mpaka umepona.

Dawa hii inakuondolea maumivu ya kichwa bila kuchelewa.

8. Chai ya kijani (Green Tea)

Chai ya kijani siyo dawa nzuri kwa ajili ya ngozi kavu tu bali pia ni moja ya dawa nzuri kabisa kwa ajili ya kutibu maumivu ya kichwa.

Chai ya kijani inaweza kukuondolea maumivu ya kichwa sababu inayo viondoa sumu (antioxidants) ambavyo vinaweza kusaidia kuondoa maumivu ya kichwa moja kwa moja.

Namna ya kutumia dawa hii:

Unahitaji:

* Maji ya uvuguvugu
* Majani ya chai ya kijani
* ½ ya limau

Hatua kwa hatua namna ya kuandaa na kutumia:

* Kwanza tumbukiza majani ya chai ya kijani ndani ya maji ya moto
* Kisha kamulia maji maji ya hiyo nusu limau ndani yake
* Mwisho kunywa chai hiyo pole pole na itakuondolea maumivu haraka mara baada tu ya kumaliza kunywa.

9. TikitiMaji

Unaweza kutumia tikitimaji kutibu maumivu yako ya kichwa. TikitiMaji pia litakusaidia kuondoa msongo wa mawazo (stress) na hivyo kufanya akili yenye utulivu.

Fanya kama ifuatavyo:

Mahitaji:

* Glasi safi
* Juisi ya tikitimaji
* Sukari

Namna ya kutumia:

* Mimina juisi ya tikitimaji kwenye glasi (ulisaga kabla ukitumia blenda bila kuondoa mbegu zake).

* Kisha ongeza kijiko kidogo kimoja cha sukari ndani yake

* Changanya vizuri na mwisho enjoy!

Kama unasumbuliwa na maumivu ya kichwa yanayosababishwa na joto lililozidi basi tikitimaji linaweza kuwa msaada mkubwa kwako.

Unaweza pia kuchanganya nusu kikombe cha mtindi, vikombe viwili vya juisi ya tikitimaji, nusu kijiko cha chai cha tangawizi iliyoparuzwa (grated), asali kidogo na nusu kikombe cha barafu.

Kisha kunywa mchanganyiko huu kuondoa maumivu ya kichwa.

10. Maji ya Kunywa

Mara nyingi kama siyo mara zote watu wanaosumbuliwa na maumivu ya kichwa wengi wao huwa ni wale wasiotilia mkazo suala la kunywa maji mengi ya kutosha kila siku.

Kichwa kuuma kina tafsiri mbili tu au sumu zimezidi au asidi ambayo nayo ni kama sumu au takataka za mwili vimezidi mwilini na ambavyo vinaweza kuondolewa kirahisi kwa kutumia maji ya kunywa tu.

Unaposikia maumivu ya kichwa chukua maji mara moja na unywe na hutakawia kuona mabadiliko mazuri.

Sasa nielewe hapa kwenye maji, maji ni mhimu kama utajiwekea utaratibu wa kunywa maji mengi kila siku na siyo mpaka uumwe kichwa.

Mambo ya mhimu kuzingatia:

Sambamba na dawa hizo hapo juu pia zingatia yafuatayo:

* Achana na mawazo (stress)
* Epuka vilevi vyote
* Oga maji ya moto
* Cheka zaidi
* Kula vyakula fresh vya asili
* Kuwa mtulivu
* Usiluke mlo wowote
* Pata muda wa kutosha wa kulala usingizi
* Kunywa maji ya kutosha kila siku lita 2 hadi 3
* Epuka vyakula kama siagi ya karanga, chokoleti, chai ya rangi, kahawa na soda nyeusi zote
* Tumia zaidi vyakula vyenye vitamin C, Vitamini B2 na madini ya magnesiamu
* Fanya masaji ya kichwa, ya shingo na ya mgongo
* Sikiliza muziki uupendao

4

rwekaza111@gmail.com

******************************************************************************************************************************************************************SASA UNAWEZA KUPATA SIMU YA IYOU MOBILE KWA MAWAKALA WOTE NCHINI

ZAIDI CLICK HAPA

19225030_142201536350706_2701361595303066560_n

Leave a comment