FAHAMU : Uvaaji wa earphone unavyoweza kukusababishia kansa

Image result for effect of using earphone
Imeelezwa kuwa watu wanaotumia redio za simu wako hatarini kupatwa na ugonjwa wa saratani ya sikio na kichwa kutokana na mionzi mikali itokanayo na viselula hivyo.
, Dk. Leopard Mwinuka alisema, watakaoathirika na tatizo hilo ni wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikioni ‘headphone’.
“Nawaonea huruma wanaotumia muda mwingi kusikiliza redio ama muziki kwa kutumia spika za masikio, kwani madhara yake hawawezi kuyaona sasa bali siku zijazo watapata ugonjwa wa saratani,” alisema Dk. Mwinuka.
Alimaliza kwa kusema kuwa, mbali na kupata ugonjwa huo, wahusika wanaweza kupata tatizo la kutosikia vizuri kwa sababu, mtu anapotumia spika za sikio huweka sauti kubwa ili apate mdundo mzuri baada ya muda ngoma ya sikio inaathiriwa na hali hiyo.
Habari nyingine za kitabibu zilisema kwamba, kwa kuwa pande zote za spika zina sumaku, huweza kuvutana na kuvuruga mpangilio wa ubongo hasa kama spika hizo zitakaa maskioni kwa zaidi ya saa nne

VILE VILE

Mbali na kundi hilo, kundi kubwa la vijana wadogo, hasa wanafunzi, pia liko katika hatari ya kupata maambukizo ya magonjwa ya masikio kutokana na mazoea hayo ya kuchangia matumizi ya spika hizo.

Watu mbalimbali waliohojiwa, wameelezea kutoelewa athari zinazoweza kusabishwa na kuchangia earphone ambazo huweza kubeba magonjwa ya ngozi na yale ya masikio kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.

Dk Kareem Segumba alisema uchangiaji wa ‘earphone’ si jambo zuri kwa kuwa husababisha maambukizi ya magonjwa mbalimbali kutoka kwa mtu mmoja aliyeathirika kwenda kwa mwingine.

“Kitaalamu tunasema anapata contagious (maambukizi) ya magonjwa ya sikio toka kwa mgonjwa. Magonjwa haya ni pamoja na fungus ya masikio,” alisema Dk Kareem.

Dk Kareem, ambaye amehudumu katika hospitali mbalimbali nchini, alitaja magonjwa mengine kuwa ni maambukizi ya sikio sehemu ya mzunguko na maambukizi kwenye ngoma ya sikio.

Image result for effect of using earphone

“Mara nyingi mtu anayeumwa fangasi ya sikio au kutokwa na majimaji kidogo kabla ya kugeuka usaha huwa hawajitambui. Wengi wanajua baada ya kuona usaha,” alisema.

“Si desturi nzuri kuchangia earphone na mtu yeyote kwa kuwa madhara yake ni makubwa na hasa ukizingatia masikio yako karibu sana na ubongo na huenda ukapata maambukizi kupitia mishipa.

“Mishipa ya damu inapeleka vijidudu vya ugonjwa kwenye ubongo na hatimaye kutokea athari nyingine kama uziwi, kupoteza nguvu ya kuona na matatizo kwenye uti wa mgongo.”

Mpigapicha wa kituo cha televisheni cha ITV mkoani Kilimanjaro, Robert Minja alikiri watu wengi hususan wanahabari wamekuwa na tabia ya kuchangia earphone, kwa vile hawajui madhara.

“Hilo la ku- share earphone (kuchangia) lipo sana na inavyoonekana watu wengi hawajui madhara yake. Tunaona ni mambo ya kawaida lakini kiukweli hii tabia ina madhara ya kiafya,” alisema.

Maulid Rashid, ambaye ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Stefano Moshi (Smmuco) alisema tatizo la kuchangia vifaa hivyo ni kubwa chuoni hapo.

“Ni kweli wanafunzi wengi wanachangia hizo earphone. Nafikiri wanaofanya hivyo hawana uelewa kuwa kuna madhara. Yaani hili ni tatizo kubwa si kwa wanafunzi tu hata watu wa kawaida,” alisema.

 

 

 

5 comments

Leave a comment