UREMBO : Jinsi ya kutengeneza hair removal wax nyumbani

[​IMG]
Chukua Kikaangio, bandika jikoni moto usiwe mkali sana, weka sukari ya kutosha.
Anza kukoroga hadi sukari ianze kuyayuka.

[​IMG]

Ikisha yeyuka vizuri chukua asali kidogo na ndimu huku ukiendelea kukoroga hadi ichemke vizuri.

[​IMG]

Kama ukiona mchanganyiko ni mzito sana ongeza maji kidogo huku ukiendelea kukoroga.
Ikishachemka vizuri, ipua na uache ipoe katika temperature ya kawaida kwa muda wa lisaa 1.

[​IMG]

Ikishapoa itakua tayari kutumia, kutunza weka katika container yako kisha weka kwenye fridge.

[​IMG]

Jinsi ya kutunza ngozi yako baada ya kuwax:

  1. Hakikisha unapaka moisturizer baada ya kufanya wax.
  2. Unaweza pia ukachukua kitamba na kukilowesha kisha kuwa kama unakanda sehemu uliyowax ili kusikakamae.
  3. Epuka kwenda juani baada tu ya ku wax, au kama inakubidi kutoka hakikisha unapaka sunscreen.
  4. Usioge kwa maji ya moto baada ya kuwax, itaondoa mafuta yako mwilini yanayofanya ngozi kuwa laini.
  5. Mahali ulipopawax pakianza kuwasha na kuwa kwekundu paka talcum powder au kanda kwa barafu.

One comment

Leave a comment