FAHAMU MAZOEZI SAHIHI KWA MAMA MJAMZITO

si kila mazoezi ni ya mama mjamzito,kuna mazoezi huruhusiwi kufanya si kwakua hautayaweza ila kwakua yanamadhara kwako na mtoto kutokana na hali uliyonayo. Hivyo mazoezi yafuatayo ni sahihi kwa mama kijacho na hayana madhara yeyote kwake na mtoto.

  • Kukimbia ; kukimbia ni mazoezi mazuri sana kwa mama mjamzito,fanya mazoezi haya kwa muda usio zidi dakina thelathini,ila pia usikimbia kwa haraka,au mwendo wa mashindano,kimbia taratibu kwa afya kwa kiwango ambacho hakitakuumiza. Usitumie nguvu kubwa katika kukimbia na hakikisha unakunywa maji ya kutosha kabla yakukimbia na baada ya kukimbia maana katika kukimbia kunakupungua maji.
  • Kuogelea ; hili ni zoezi zuri sana pia kwa mama mjamzito,ni zoezi litakalo kusaidia kua mwepesi zaidi na pia litakusaidia kuwa na utulivu (relaxation) maana akili itakua katika utulivu na hapa ndo matokeo ya kutokua katika msongo wa mawazo yanapatikana. Pia itakusaidia viungo vyako kuwa katika hali nzuri zaidi itakayo leta manufaa wakati wako wakujifungua.
  • Kutembea ; kutembea pia ni mazoezi mazuri sana, wamama wengi wajawazito wanatabia yakukaa kizembe nyumbani na kuruhusu hali ya kuchoka choka kuwatala na kua wavivu nyumbani,wakilala nakuamka au kukaa sehemu moja wakijua ndo njia sahihi yakumlinda kiumbe ndani yake ila yapo manufaa makubwa sana wakati mama kijacho anafanya mazoezi yakutembea. Toka nje tembea,fanya hata matembezi ya jioni,wakati ambapo hapana jua kali,na tembea barabara ambayo haina mashimo shimo na maporomoko,wakati wa matembezi viungo vyako vya mwili vitakua imara zaidi na pia utamsaidia mtoto katika mzunguko wake. Afya yako ina muathiri mtoto pia hivyo usikubali kukaa kizembe.
  • Yoga ; Ni mazoezi mengine mazuri sana ambayo hutumika kwenye mataifa mengi ambayo chanzo chake ni kutoka kwa wahindi (Buddha) ila ni mazoezi yanayoshauriwa sana kwa mama wajawazito. Ni mazoezi salama na yenye matokeo mazuri,husaidia kwenye swala zima la viungo na pia kwenye swala zima la upumuaji. Mama mjamzito anahitaji sana kua na pumzi nzuri hususani wakati ule atakua katika kujifungua hivyo inabidi sana kuangalia swala nzima la pumzi yako na yoga husaidia sana.
  • Kucheza muziki ; mmmh hapa ni pazuri sana tena ikiwezekana kama uwezo upo jisajili kwenye vikundi vya wamama wajawazito ambao hukutana pamoja nakufanya mazoezi pamoja,maana kwenye kucheza mziki wakikundi kuna kuongezeka kwa furaha,akili inatulia sana na zaidi viungo vyako vinakua katika mazoezi. Hakikisha unakua mama kijacho fit.

Hayo ni baadhi ya mazoezi ambayo ni salama sana kwa mama mjamzito, yapo mazoezi mengine mengi ila lazima uhakikishe unaelewa matokeo ya mazoezi hayo kwenye mwili wako kabla hujaanza kufanya. Ila pia yapo mazoezi ambayo kama mama mjamzoto haishauriwi kuyafanya naamini katika makala nyingine tutapata maarifa hayo. Uwe na wakati mwema mpaka wakati mwingine tena. Kumbuka afya yako ni yamuhimu sana kwa ajili yako ila pia kwa ajili ya kiumbe ndani yako.

Leave a comment