UREMBO: HII NDIO STREAMING ASILIA KWA UBORA WA NYWERE ZAKO

Habarini??

Natumaini mu wazima, Leo ngoja tujadili kidogo steaming asilia ambayo unaitengeneza mwenyewe na kuboresha afya na muonekano Wa nywele zako

Mahitaji;-
parachichi
yai la kuku Wa kienyeji
Asali

hatua;- chukua parachichi lako likate toa ile nyama ya ndani weka kwenye chombo ili utengeneze mchanganyiko wako

ii/;- chukua yai lako pasua chukua kiini tu cha yai lako changanya na parachichi

iii/;-chukua asali yako pima vijiko viwili au vitatu vikubwa changanya kwenye ule mchanganyiko koroga Hadi vyote vichanganyike vizuri

Baada ya hapo osha nywele zako pakaa huo mchanganyiko na ukae kwenye steamer mda kadhaa
na baadae uzioshe hapo utakuwa umeboresha nywele zako kiasili zaidi ni hayo tu!!!13741394_989498261148675_1055343028_n.jpg

Leave a comment