SPORTPESA YATIMIZA NDOTO ZA WATANZANIA 20 KUPITIA PROMOSHENI YA KUSHINDA BAJAJI

 

Promosheni ya Jiongeze na M-Pesa, Shindana SportPesa imefikia tamati siku ya Alhamisi ya April 19 na kushuhudia watanzania 20 kutoka mikoa mbalimbali wakijishindia bajaji aina ya TVS KING.

Promosheni hiyo iliyokuwa ikiendeshwa na kampuni ya michezo ya kubashiri ya SportPesa wakishirikiana na Vodacom kupitia huduma ya M-Pesa ilizinduliwa rasmi siku ya Februari 9 mwaka huu kwenye viwanja vya Zakiem, Mbagala jijini Dar es Salaam.

Katika promosheni hiyo iliyodumu kwa wiki kumi, washindi wawili walikuwa wakijinyakulia bajaji mpya kila wiki katika droo zilizokuwa zikichezeshwa siku za Jumatatu na Alhamisi zikisimamiwa na bodi ya michezo ya kubahatisha nchini.

Kwa mara nyingine tena tumeshuhudia SportPesa wakiendelea kuwainua watanzania kiuchumi huku promosheni hii ikiwa ni muendelezo wa ile promosheni ya kwanza iliyodumu kwa siku mia moja ambayo ilikwenda kwa jina la ShindanaSportPesa.

Washindi

Jumla ya washindi 20 wamepatikana kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania ambapo Bwana DaudiSima (36) kutoka Makete Njombe ndiye alifungua dimba kwenye drooya kwanza iliyofanyika Februari 12 na baada ya hapo washindi wengine walifuata ambao ni Edwin Victor (23), AggreyLauwo (19), Godfrey Magesa (37), Enock Sagwa (32), Yohana William (28), Richard Steven (23), ErastoFloridi (22), Joseph Nzary (32) na Gerald Christopher (25).

Wengineni Paschal Raphael (24), Mathayo Edward (27), Majaliwa Hassan (29), Yohana Msigala (22), JumaTwike (35), John Mawela (32). Karim Prosper (29), Adam Obura (34), Linda Mwandu (32) na AwadhHussein (28) ambaye ndiye amefunga dimba.

Mwanza yaburuza

Mkoa wa Mwanza umeongoza kwa kutoa washindi wengi (4) ukifuatiwa kwa ukaribu na mkoa wa Mara wenye jumla ya washindi watatu, kisha mikoa ya Dar es Salaam, Rukwa, Kagerana Iringa yenye washindi wawili kila mmoja na bila kusahau Mbeya, Ruvuma, Njombe, Shinyangana Kilimanjaro yenye mshindi mmoja mmoja.

Ndotokuwakweli

Wakati wa kukabidhi bajaji ambazo zilikuwa zikipelekwa na SportPesa hadi nyumbani kwa washindi, washindi wote walieleza jinsi ambavyo bajaji hizo zitaweza kuwakwamua kiuchumi.

Yohana William (28)kutoka Mwanza nimuuza kuku katika soko la Igoma nayeye kwa upande wake anaamini ataweza kutimiza ndoto zake kupitia ushindi huo.

Leave a comment